Tanzania ni Miongoni mwa nchi 191 zinazoshiriki kwenye Maonesho ya Dunia ya EXPO2020 Dubai ambayo yameanza rasmi tarehe 01 Oktoba, 2021 na yanatarajia kumalizika tarehe 31 Machi, 2022. Ushiriki wa Tanzania unaratibiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini UAE, Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi.
Kaulimbiu Kuu ya Maonesho haya ni “Connecting Minds, Creating the Future”, inayolenga kuleta fikra za dunia pamoja kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili. Tanzania inashiriki katika eneo la Mobility yenye kauli mbiu ndogo isemayo
“Connectivity, Tanzania Ready for Take Off” ambayo inaonesha utayari wa Tanzania kuwa Kitovu cha Biashara Barani Afrika kwa kuiunganisha Afrika na Dunia.